Importance announcement

Makamo mwenyekiti wa jumuiya ya ZAGCO Mhe Khamis Haji Mbwembwe na Katibu mkuu wa ZAGCO Mhe Yussuf Ali Suleiman wanawataarifu kikao cha kamati ya utendaji ZAGCO kitakachofanyika siku ya Ijumaa sawa na tarehe 22/ 8/2025 saa 9:00 jioni Mjini VUGA kampasi ya SUZA ni muhimu kwa viongozi wote kufika.

Wahusika wa mkutano huo ni kama katiba inavoeleza manaibu katibu wakuu wote unguja na pemba , wajumbe wawili wateule, wenyeviti na makatibu wa kamati ndogondogo wote, mshika hadhina , pia mualiko maalum kwa mwenyekiti katibu na mshika fedha wa kamati ya maonyesho ukipata taarifa hii mjulishe na mwanzako

AGENDA KUU ZA MKUTANO HUU

  1. kupokea report ya maonyesho kwa ujumla wake kutoka kwa kamati
  2. kujadili tarehe ya mkutano mkuu
  3. kuteuwa kamati ya uchaguzi ZAGCO
  4. kupitisha tarehe ya mkutano wa bodi ya wadhamini

Mwisho mwenyekiti wa jumuiya ya ZAGCO anawaomba viongozi wote kwa ushirikiano mkubwa tuweze kuhudhuria kwa wakati uliopangwa

Ahsanteni

Imeandaliwa na ofisi ya Katibu mkuu ZAGCO

Leave A Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *