Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya vijana Zanzibar Mhe Shaib Ibrahim Muhamed ametembelea taasisi ya ZAGCO kwa lengo la kuangalia shughuli zinazofanyika pamoja na changamoto zinazowakabili katika eneo la maonyesho Dole Kizimbani Unguja na eneo la kilimo Kizmbani Pedock.
Mhe Shaibu amewaasa wataalamu hao kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu katika kutumia vizuri maeneo yaliyopo kwa shughuli za kilimo na mifugo, hii itaongeza ari kwa vijana walioko nje kuona umuhimu na fursa za ajira zilizokuwepo katika tasnia izo.
Nae mkurugenzi wa ZAGCO akizungumzia changamoto zilizopo ni pamoja na ukosefu wa miundombinu imara katika shamba hilo hasa mifumo ya umwagiliaji.