Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar. Dkt. Salum Soud Hamed, amefungua mafunzo ya wakulima na kuzindua mbegu mpya ya mahindi aina ya Sugar King F1 (Sweet Corn) huko Dole, Kizimbani, Viwanja vya Maonesho Zanzibar.
Pia ameipongeza ZAGCO pamoja na kampuni ya EAST WEST SEED TANZANIA kwa juhudi zao katika kuwawezesha wakulima kupitia mbinu bora za uzalishaji.
Washiriki wa mafunzo hayo ni wanafunzi wa SUZA Skuli ya Kilimo Kizimbani, wakulima, wakufunzi, wanachama wa Jumuiya ya ZAGCO pamoja na kampuni ya East West Seed.