ZAGCO haipo nyuma kwenye kuadhimisha maonesho ya Nane Nane

Shirika la Zanzibar Green Culture Organization (ZAGCO) liliendesha warsha maalum ya kutoa elimu inayohusiana na aina mbalimbali za mazao ya mboga mboga. Wanafunzi kutoka skuli mbali mbali walipata fursa ya kujifunza kwa vitendo kuhusu kilimo hai, utunzaji wa mimea, na umuhimu wa bustani za mboga mboga kwa lishe bora na mazingira endelevu. Wakiwa chini ya maelekezo ya wataalamu wa ZAGCO, wanafunzi walishiriki kwa hamasa kuuliza maswali, kuandika dondoo, na kushuhudia mbinu bora za kilimo hai zinazolenga kulinda mazingira na kuimarisha afya za jamii.

Leave A Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *